Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kama ifuatavyo:-
1. Walinzi Daraja la III “Nafasi 6” Unguja na “Nafasi 3” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya Ulinzi (Mgambo au JKU au JKT)
2. Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
3. Afisa Takwimu Daraja la II “Nafasi 2” Unguja na “Nafasi 2” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Takwimu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
4. Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi na Mipango kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
5. Waandishi wa Habari Daraja la II “Nafasi 2” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Uandishi wa Habari kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
6. Mtunza Picha Daraja la III “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ya Upigaji Picha au Uandishi wa Habari kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
7. Fundi P.A Daraja la III “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ya ‘Electric and Telecommunication Enginering’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
8. Mpiga Picha Daraja la III “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ya Uandishi wa Habari au Upigaji Picha kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
9. Watunza Nyaraka Daraja la III “Nafasi 2” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
10. Afisa Uhuishaji Nyaraka Daraja la II “Nafasi 2” Unguja na “Nafasi 2” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Record Management’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
11. Dereva Daraja la III “Nafasi 1” Unguja na “Nafasi 2 Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kupata Cheti cha Udereva na leseni hai Class ‘C’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
12. Wahudumu wa Maeneo ya Kihistoria Daraja la III “Nafasi 4” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Stashahada katika fani ya Utamaduni na Urithi ‘Culture and Haritage Management’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
13. Muhifadhi wa Vitu vya Kale Daraja la II “Nafasi 1” Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Historia kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
14. Akiolojia Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza ya Akiolojia kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
15. Wahudumu Daraja la III “Nafasi 4” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amemaliza elimu ya Sekondari.
16. Afisa Utalii Wilaya Daraja la II “Nafasi 7” Unguja na “Nafasi 4” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Utalii kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
17. Afisa Utafiti Daraja la II “Nafasi 1” Unguja na “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi na Mipango kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
18. Afisa Utalii Mkoa Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Utalii kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
19. Afisa Utumishi Mkoa Daraja la II “Nafasi 1” Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala wa Umma kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587,
ZANZIBAR.
• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba. Muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoiomba vyenginevyo maombi yake hayatazingatiwa.
Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 21 Juni, 2019 wakati wa saa za kazi.
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA BONYEZA HAPA CHINI 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI KATIKA WIZARA YA HABARI,UTALII NA MAMBO YA KALE-ZANZIBAR
Reviewed by kidebwaymnyama media
on
June 16, 2019
Rating:
No comments: